Monday, July 29, 2013

Hili NDILO JIWE LA AJABU NCHINI TANZANIA NA HAIRUHUSIWI KULIPANDA WALA KULISOGELEA!!

Haya ndio maajabu ya JIWE LA MBUJI wilayani Mbinga, Ruvuma.

Maana ya neno "MBUJI" ni "Kitu Kikubwa"
  1. Baada ya utafiti wa mkoa wa Ruvuma, ndilo jiwe pekee kubwa mkoani humo.
  2. Lina vyanzo vingi vya maji
  3. Huwezi kulipanda mpaka uombe kibali kutoka kijijini hapo. Na ukithubutu kulipanda bila ya ruhusa, unaweza ukafa. Na tayari kuna Mzungu mmoja alikuja kwaajili ya utali, akapanda hilo jiwe bila idhini na akakutwa amepoteza maisha.
  4. Ni vigumu kulizunguka. Unaweza ukazunguka na usifike mwisho, hata kama uliweka alama, hutoikuta.
  5. Jiwe la Mbuji hutumika kwaajili ya matambiko kwa baadhi ya koo za eneo hilo.
  6. Kuna watu maalumu wanaotoa maelekezo kwa yeyote anaetaka kulisogelea au kulipanda.
  7. Ni kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea vijiji vya Litembo, Maguu, Hagati nk. huko Mbinga, Ruvuma.
  8. Linaheshimika sana kwa wakazi wanaolizunguka jiwe hilo.
  9. Sehemu kubwa ya watu wanaoishi karibu na jiwe hilo, hawajawahi kulizunguka wala kulipanda kutokana na hofu.
  10. Jina la jiwe hilo ndio tarafa ya Mbuji wilayani Mbinga.
 ********************************************************************************

These are the wonders of Mbuji stone, Mbinga District, Ruvuma, Tanzania.

The meaning of the word "Mbuji" is "Something Big"

  1. After research on Ruvuma region, it is  the region's biggest stone. 
  2. Has many sources of water.
  3. You  cannot climb till you request permission from the village. And if you dare climb without permission, you can die. And already there is a European who came in favor of tourism, climbed the rock without permission and he was found dead.
  4. You can  hardly circle the rock. Also, you can go around and do not bar the end, even if you leave a mark. 
  5. Mbuji stone is used for rituals in favor of some of the families of the area.
  6. There are special people who give instructions to anyone who wants to climb the stone. 
  7. It is a major attraction for visitors who visits Litembo, feet, Hagati villages etc. in Mbinga District, Ruvuma, Tanzania.
  8. The stone is very respected by the people around the area.
  9. A large proportion of people living near that stone, out of fear, they have neither climbed nor circled the stone.
  10. Name of the stone is the division of  Mbuji, Mbinga District.

HATIMAYE MBOWE AWASILISHA USHAHIDI POLISI KUHUSU MLIPUAJI WA BOMU ARUSHA

HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, jana amewasilisha kwa maandishi ushahidi wake makao makuu ya Jeshi la Polisi mjini Dar es Salaam.

Maelezo ya Mbowe ambayo jana yaliwasilishwa, yamekuwa siri nzito, kwani yanatokana na msimamo wa CHADEMA kudai wana ushahidi na tukio la mauaji ya mlipuko wa bomu lililotokea Juni 15, mwaka huu mkoani Arusha.
 
Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala alilithibitishia MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, kuwa aliwasilisha saa 5 asubuhi ambapo alipokelewa na Mkuu wa Idara ya Operesheni za Upelelezi Tanzania (CID), Kamishna Advocate Nyombi.

Baada ya kuwasilisha maelezo hayo, Wakili Kibatala alikataa katakata kuzungumzia kilichomo ndani ya maandishi hayo, kwa madai kuwa ni siri yao na polisi.

“Nathibitisha bila shaka, nimewasilisha majibu kwa niaba ya Mbowe leo (jana), makao makuu ya polisi kama tulivyokubaliana, lakini yaliyoandikwa humo ni siri…siwezi kuzijadili tusubiri kutoka kwao,” alisema Kibatala.

Hatua ya kuwasilisha majibu hayo kimaandishi, ilifikiwa Jumatano wiki hii katika mahojiano baina ya Polisi na Mbowe.

Siku hiyo, Mbowe aligoma kuwasilisha ushahidi wake polisi kama alivyotakiwa kwenye barua aliyoandikiwa na jeshi hilo Julai 17, mwaka huu, kwa kile alichosema hadi Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji kuchunguza tukio hilo.

Katika barua hiyo, Mbowe alitakiwa kufika bila kukosa akiwa na ushahidi wa mauaji ya mlipuko wa bomu hilo.

Hata hivyo, Mbowe aliripoti kuitikia wito wa barua hiyo, lakini aliendelea kushikilia msimamo wake wa kutowasilisha ushahidi huo kwa polisi.

Jeshi la Polisi, limekuwa katika mvutano na Mbowe likimtaka kuwasilisha ushahidi kuhusu mlipuko wa bomu hilo, katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nne na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 70, katika uwanja huo ushahidi ambao alidai anao.

Endapo Mbowe atakutwa na hatia ya kutokuwa na ushahidi huo, atakumbwa na adhabu ya miaka mitatu jela au faini ya Sh 500,000.

Hii ni kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika barua yake kwa Mbowe, ikunukuu kifungu cha sheria ya kifungu cha 10(2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura ya 20, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002

Tuesday, July 2, 2013

Kifuta Jasho


Mpango wa AGOA ulioiingizia Tanzania Sh92.8trilioni

Wafanyabiashara Tanzania watumia asilimia 8

Ukuzaji fursa za kiuchumi Afrika, (African Growth and Opportunity Act), AGOA, ni mpango mahsusi ulioanzishwa kwa ajili ya kuziwezesha nchi za Afrika kuuza bidhaa zao nchini Marekani.

Mpango huo upo kwa mujibu wa sheria baada ya kupitishwa Mei 18, 2000 na kwamba mpango huo unasaidia nchi za Afrika ikiwamo Tanzania kuuza bidhaa zao, kukuza mitaji pamoja na kupanua masoko kiuchumi.

Aliyekuwa Rais wa Marekani, George W. Bush alitia saini Mkataba wa Biashara kati ya Mataifa ya Afrika na Amerika, kupitia AGOA mwaka 2004.

Tanzania ambayo ni mmoja wa wanachama wa AGOA, ni miongoni mwa nchi zinazofaidika na mpango huo kwa kuuza bidhaa mbalimbali Marekani na kuingiza Sh92.8 trilioni hadi mwaka 2011, ikiwa ni zaidi ya asilimia 36.

Mwaka 2010, mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani yaliingiza Dola 15 milioni (Sh24 bilioni) ikiwa ni juu ya asilimia 73.1 tangu mwaka 2000.

Makubaliano ya biashara

 Mbali na mpango wa AGOA, Marekani ilisaini mkataba uitwao; Trade and Investment Framework Agreements (TIFA) na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2008, na Soko la Pamoja kwa Nchi za Kusini na Mashariki (Comesa) mwaka 2001. Tanzania ni mwanachama wa jumuiya zote hizo.

Marekani imekuwa ikijaribu mpango wake wa biashara na Afrika Mashariki na hata mwakilishi wake, katika masuala ya biashara Balozi, Ron Kirk aliwahi kuitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka huo, 2011 lengo ni kuimarisha uhusiano wa biashara kati ya Tanzania na Marekani.

Tanzania ni kati ya mataifa 136 yanayofanya biashara na Marekani na tangu kipindi hicho, jumla ya biashara za kuuza na kununua zinafikia Dola 316 milioni. Tanzania ni nchi ya 121 inayosafirisha kwa wingi bidhaa zake kwenda Marekani.

Kwa mwaka 2011, Marekani iliuza bidhaa zake Tanzania zenye thamani ya Dola 258 milioni, sawa na asilimia 57.7, ikiwa ni zaidi ya Dola 94 milioni tangu mwaka 2010, na zaidi ya asilimia 474.7 tangu  mwaka 2000.

Nchi hiyo pia imenunua kutoka Tanzania mashine mbalimbali za Dola 61 milioni, ngano (Dola 53 milioni), bidhaa za nguo (Dola25 milioni), mpira (Dola 15 milioni), na mashine za umeme za Dola 13 milioni.
Kwa mazao ya kilimo, Marekani ilinunua; kahawa, viungo, chai zilizoliingizia taifa Dola 29 milioni, madini (Dola 9 milioni, Knit Apparel Dola 5 milioni), mbogamboga ziliingiza Dola 5 milioni, matunda, korosho Dola 2 milioni na kahawa iliyoingiza Dola 28 milioni.

Kimsingi, Marekani na Tanzania ni washirika wakubwa katika biashara hasa katika Ukanda wa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Nchi hiyo iko katika harakati za kuwekeza kupitia mpango wake wa Millennium Challenge Account, Feed the Future na Partnership for Growth (PFG).

PFG, ni mpango wa kwanza wa Rais Barack Obama kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi zinazoendelea, demokrasia na utawala bora.

Nafasi za biashara

 Pamoja na kuwapo kwa nafasi za kuuza bidhaa mbalimbali nchini Marekani kupitia AGOA, wafanyabiashara wanatumia asilimia nane pungufu ya nafasi zinazotolewa na Marekani.

Kutokana na hali hiyo, Serikali inawataka wafanyabiashara kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya kukuza kipato chao na cha taifa kwa kufanya biashara na taifa hilo lililostawi kiuchumi.

Akizungumza kwenye Mkutano wa mwaka wa TCCIA, Juni mwaka huu, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk  Abdallah Kigoda, anasema pamoja na kuwepo wigo mpana wa biashara kama; AGOA, Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC), Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afika (Sadc), Tanzania inashiriki katika Jumuiya hizi katika nafasi ndogo.

 “Ni wakati wa wafanyabiashara kuzalisha mali kwa wingi na bora, kisha kuuza nje ikiwamo katika jumuiya mbalimbali zenye wigo mpana wa biashara,” anasema Dk Kigoda.

Dk Kigoda anasema, TCCIA lazima itoe elimu kwa wanachama wake, hasa kuhusu umuhimu wa uzalishaji na usindikaji mali ulio bora na kuuza nje ili kuongeza pato kwa mkulima kwa mazao bora.

Uwekezaji wa Marekani Tanzania

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC, Raymond Mbilinyi anasema  uwekezaji wa taasisi za nje nchini, umekua kwa asilimia 10 na ulitarajiwa kuingiza Dola13 bilioni hadi kufikia mwishoni mwa 2012.

Hata hivyo, China inaonekana kuteka sehemu kubwa ya uwekezaji Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania ikilinganishwa na Marekani. Mpaka sasa, China imewekeza Dola1.4 bilioni ikiwa ni zaidi ya Marekani ambayo imewekeza Dola950 milioni Tanzania.

Ujio wa Rais Barack Obama  leo unaweza kuongeza wigo wa nchi yake kuwekeza Tanzania hasa kupitia mpango wa Millennium Challenge Corporation, MCC.

Akithibitisha hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anasema uwekezaji utaongezeka kupitia mpango wa MCC, ambao utafadhili masuala ya elimu, afya na miradi ya barabara.

MCC, ni mpango ulioasisiwa na Baraza la Congress la Marekani mwaka 2004 kwa ajili ya kusaidia nchi zinazoendelea, na mwaka 2011 uliisaidia Tanzania Dola 698 milioni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Tanzania imekuwa ikipata misaada ya MCC kwa elimu, miundombinu na afya...tutafanya mazungumzo kuhusu masuala ya kiuchumi, nishati Afrika na maendeleo ya uchumi na jinsi ya njia mbalimbali za uwekezaji.”

Mpango mwingine uliopo katika kukuza uchumi ni kupitia Millennium Challenge Account, MCA, ambao kazi yake ni kuendeleza sekta ya usafiri, umeme na maji.

Obama, Bush ana kwa ana Tanzania

Rais wa Marekani, Barack Obama na mtangulizi wake, George W. Bush, leo wanakutana ana kwa ana kwenye ardhi ya Tanzania watakapoweka mashada kwenye Ubalozi wa zamani wa Marekani uliolipuliwa mwaka 1998.

Rais Obama ameweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza mweusi kuchaguliwa kuongoza Marekani, akipokea wadhifa huo kutoka kwa Rais Bush, ambaye aliiongoza taifa hilo kuanzia mwaka 2000-2008.

Kitendo cha vigogo hao kukutana nchini ni cha kihistoria na kinadhihirisha jinsi Marekani ilivyoipa kipaumbele Tanzania kwa masuala ya diplomasia.
Viongozi hao wawili, wapo Tanzania wakati Rais Obama akimalizia ziara yake ya Afrika na Bush atakuwa na mkewe, Laura, watahudhuria mkutano wa wake za marais wa Afrika unaodhaminiwa na Taasisi ya Bush Foundation.

Pia, Michelle Obama, atahudhuria mkutano huo kabla ya kuondoka kurejea Marekani.
Balozi mbili za Marekani za Dar es Salaam na Nairobi, Kenya zilishambuliwa kwa wakati mmoja Agosti 7, 1998. Obama ataweka shada kama sehemu ya kumbukumbu ya tukio hilo na Bush ataungana naye katika shughuli hiyo.

Hata hivyo, viongozi hao hawatahutubia wakati wa shughuli hiyo.
Rais Obama ametoa pongezi kwa sera za Bush Afrika hasa kwa kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Hata hivyo, utawala wa Rais Obama umejikita zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Kuna kamandi ya Jeshi ya Africom, ambayo ina kazi kubwa ya kukabiliana na ugaidi barani humu.Operesheni kubwa za Africom zipo nchi za Afrika Kaskazini, Somalia na Afrika ya Kati ambako wanamsaka kiongozi wa Kundi la Waasi la Lord Resistance, Joseph Kony.

Monday, July 1, 2013

Obama awasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius K. Nyerere Dar Es Salaam majira ya saa nane na dakika arobaini mchana

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania leo Jumatatu, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.

Akiwa nchini Tanzania rais Obama atafanya mazungumzo na rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete  na waandishi wa habari na kisha kutembelea kituo cha umeme cha Ubungo , baada ya kuahidi kutoa dola za Marekani bilioni saba kusaidia mradi wa umeme Barabi Afrika.

Mpango huo wa serikali ya Marekani utazinduliwa kwanza katika nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania ambazo wananchi wake wanakumbwa na matatizo ya upatikanaji wa umeme.

Aidha Obama ameeleza kuwa Afrika itakuwa na mustakabali mzuri kwa kuwa na viongozi wanaopambana kuhakikisha raia wao wanakuwa na maisha bora.
Katika ziara yake nchini Afrika Kusini , Obama hakusita kusifu jitihada za kiongozi wa zamani na baba wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye ameeleza kuwa jitihada zake za ukombozi kwa raia wa taifa hilo zilimsukuma kuingia katika siasa na hatimaye kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani