Friday, May 31, 2013

Rest In Peace Albert Mangwea a.k.a Ngwair, Cowbama, Cowwizy..

NDUGU wadau wa blogu ya Hot92tanzania.blogspot.com tunaomba radhi kwa kuwaletea picha hii ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea, aliyefariki Dunia juzi nchini Afrika Kusini,tunatambuwa kuwa picha hii si nzuri lakini tumelazimika kuwaletea ili mshuhudie jinsi mpendwa wetu alivyokuwa kabla ya kutengenezwa.
Kiukweli Mangwea alikufa kifo cha masikitiko, msanii huyo aliyewai kutamba na wimbo wa Geto langu pamoja na mikasi iliyotengenezwa na mwaandaaji wa ala za muziki nchini Tanzania P Funk Majani.
Mangwea alikutwa amekufa katika chumba walichokuwa wamelala na msanii wa mwenzake M 2 The P, Mangwea alikutwa amelowa damu nyingi, ambazo zilikuwa zikitoka kwa wingi kupitia mdomoni,puani na masikioni.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Hot92tanzania.blogspot.com kwamba kitendo cha msanii huyo kuvuja damu nyingi ndiyo iliyosababisha kifo chake na kwamba hata jopo la Madaktari waliompokea walishangazwa na damu hizo kabla ya uchunguzi kufanyika.

Kwa upande mwingine, mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
"Tumeamua kwa mikono miwili kushiriki katika msiba huu wa ndugu yetu Mangwea,” alisema kwa ufupi. Ngwea amepangwa kuletwa Tanzania kesho Jumamosi na kuagwa Jumapili, kabla ya kupelekwa mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake.

  Barua inayoonyesha walioanza kuchangia msiba wa Ngwea.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
 
KAMPUNI ya Clouds FM, imejitolea kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwea kwa ajili ya kuutoa Afrika Kusini hadi Tanzania kwa ajili ya kuzikwa, ukiwa ni utaratibu unaoonyesha kuwa wadau wote wameamua kushirikiana katika suala hili.

Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, alithibitisha kuchukua uamuzi huo kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya nyota huyo wa Bongo Fleva.

No comments: