Tume
ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa
itafanya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
siku ya Jumatatu, Juni 3, 2013, kuanzia saa 8:00 mchana katika viwanja
vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi
huo utarushwa moja kwa moja na vituo vya redio vya TBC Taifa, ZBC Redio
na vituo vya televisheni vya TBC 1 na ZBC TV na vituo vinginevyo vya
redio na televisheni.
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu za mikononi (sms) na nyinginezo.

Tume inawaomba wananchi na wadau kufuatilia uzinduzi huo kwa makini kupitia vyombo hivyo vya habari.
Mwisho.
Mwisho.
Imetolewa na:
Noel Kapinga Jr.
No comments:
Post a Comment