Kauli hiyo iliyotoka leo majira ya saa tatu asubuhi, imeleta maswali mengi miongoni mwa watanzania. Wengi wanajiuliza ni kwanini mwili wake uhairishwe kusafirishwa mara ya pili, iwapo haijatolewa sababu yoyote ya msingi.
Safari ya kwanza ya kuuleta mwili wa marehemu ngwair ilikuwa ni jumamosi lakini wakahairisha kutokana na maombi ya kuuga mwili huo kwa watanzania waishio Afrika kusini, na kusema unaweza kusafirishwa leo na kuingia saa nane mchana kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Aiport jijini Dar Es Salaam. Napo hiyo safari imehairishwa na kupanga kesho ndio mwili huo unaletwa Tanzania.
Sababu iliyotoka ni kwamba wanahofia usalama wa safari yenyewe kitu ambacho si cha msingi. Na kuleta maswali mengi kuto kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam.
"Mimi nahisi kuwa mwili wa mshikaji wetu (ngwair) umebaki tena labda kwaajili ya uchunguzi wa madaktari, koz inaweza ikawa jamaa aliwekewa sumu, hivyo basi wamembakiza huko ili wafanye uchunguzi huo" alisema mkazi mmoja wa mitaa ya sinza kumekucha (jina limehifadhiwa).
Je! hii ni kwa sababu gani??
No comments:
Post a Comment